Tanzania yapunguza vifo vya wajawazito kwa asilimia 21

23 Septemba 2013

Katika kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia hususani lengo la tano la kupunguza vifo vya wajawazito, serikali yaTanzaniakupitia wizara ya afya inasema imepunguza vifo hivyo hivyo. Takwimu za wizara ya afya zinaonyesha kuwa vifo vya wajawazito vimepungua kwa asilimia 21 kutoka vifo 578  kwa kila uzazi hai Laki Moja kati ya mwaka 2004-2005 hadi vifo 454 kwa kiwango hicho kati ya mwaka 2009 hadi 2010. Benedicto Ngaiza ni Mganga Mafawidhi  katika  hospitali ya rufaa mkoani Ruvuma na anaeleza mikakati ya hospitali hiyo katika kutimizahilo

(Sauti ya Benedicto)

Mengi zaidi juu ya kupunguza vifo vya kina mama wajawazito nchiniTanzaniautayasikia katika makala hivi punde

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter