Ban alaani shambulizi la kigaidi Nairobi

22 Septemba 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon, amelaani vikali shambulizi la kigaidi lililotekelezwa Jumamosi mjini Nairobi, Kenya, ambalo liliwaua watu kadhaa na kuwajeruhi wengine wengi. Bwana Ban amesema kitendo hicho cha kupangwa na ambacho kiliwalenga raia wasio na hatia, ni cha kukemewa na kisichokubalika.

Katibu Mkuu ametuma risala za rambi rambi kwa familia za wahanga na majeruhi wakiwemo watu kutoka nchi zingine, pamoja na Rais Uhuru Kenyatta, ambaye ameongea naye kwa njia ya simu mnamo siku ya Jumamosi.

Bwana Ban amesema waliohusika katika kutekeleza shambulizi hilo ni lazima wakabiliwe kisheria haraka iwezekanavyo.

Nairobi ni makao makuu ya Umoja wa Mataifa barani Afrika, na kuna mamia ya wafanyakazi wa kitaifa na wa kimataifa. Ninasikitika kuripoti kuwa mfanyakazi mstahafu wa UNICEF alikuwa miongoni mwa wale walouawa. Nimezungumza na Rais Kenyata na ninaendelea kuwasiliana na Mkurugenzi Mkuu wa Umoja wa Mataifa mjini Nairobi, Bi Sahle-Work Zewde wakati hali hii  ya dharura inapoendelea kubainika.

Bwana Ban amesema huu ni wakati wa mshtuko mkubwa kwa Wakenya wote, pamoja na Umoja wa Mataifa, na kuongeza kuwa Umoja wa Mataifa unasimama bega kwa bega Ma watu wa Kenya wakati huu.