Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Migomo ya elimu iepukwe kunusuru mustakabali wa elimu:UNESCO

Migomo ya elimu iepukwe kunusuru mustakabali wa elimu:UNESCO

Migomo katika sekta ya elimu hudidimiza kiwango cha elimu katika eneo husika na hivyo kuzorotesha maendeleo, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO. Katika kuangazia hili afisa wa UNESCO nchini Tanzania Elizabeth Kyondo anasema ni muhimu mazingira ya walimu yakaboreshwa ili wafanye kazi zao kwa ufanisi ili kuleta tija katika mustakabali wa elimu hususani shule ya msingi. Ungana na Joseph Msami pamoja na Victor Kibego wa radio washirika ya Spice FM nchini Uganda, katika makala inayomulika mgomo wa waalimu wa shule za msingi nchini Uganda na athari zake.