Mshoromoni Mombasa, Kenya na harakati za kupambana na Ukimwi

20 Septemba 2013

Ripoti mpya ya mfuko wa kimataifa wa kupambana na Ukimwi, Malaria na Kifua Kikuu, Global Fund imesema mafanikio makubwa yamepatikana katika kupambana na magonjwa hayo. Kubwa zaidi ni utoaji wa dawa za kupunguza makali ya virusi hivyo kwa makundi mbali mbali mbali ikiwemo wajawazito, elimu ya kinga na kadhalika. Mafaniko hayo yametangazwa wakati huu ambapo wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa watakutana hapa New York kuanzia wiki ijayo kutathimini malengo ya Milenia ikiwemo lile la tiba dhidi ya magonjwa ikiwemo Ukimwi na Malaria.

Huko Mshoromoni, Mombasa nchini Kenya, harakati mbali mbali zinachukuliwa kujikinga na ugonjwa huo. Basi ungana na Salim Chiro kutoka radio washirika ya Pwani FM huko Mombasa kufahamu kile kinachofanyika na ujasiri wa wale wanaoishi na virusi vya Ukimwi wa kutokata tamaa.

(Makala ya  Salim Chiro)