WFP yahofia hali watu walonaswa katikati ya mapigano Syria

20 Septemba 2013

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limesema kuwa limeingiwa na wasiwasi kufuatia idadi kubwa ya watu kunaswa katika miji ya Syria ikiwemo Damascus katika wakati ambapo mapigano yakiendelea kuchacha.

WFP imeanzisha juhudi za kusambaza misaada ya chakula kwa watu zaidi ya milioni 3 katika kipindi cha mwezi huu na tayari imetoa mwito kwa pande zinazopigana kuruhusu shughuli za usambazaji wa chakula kufanyika kwa usalama.

Ripoti zinasema kuwa, WFP imekuwa ikifanya kazi katika mazingira magumu kutokana na kukosekana kwa hali ya usalama. Tangu kuanza kwa mwaka huu, WFP imerekodi matukio yanayokaribia 50 yanayohusika na upotevu wa mizigo yake.