Machafuko mapya yazuka CAR

20 Septemba 2013

Ripoti kutoka Jamhuri ya Kati zinasema kuwa, mamia ya watu wamekosa makazi kutokana na mapigano yaliyoibuka upya katika eneo la Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo.

Mapigano hayo yameripotiwa kuibuka siku ya jumamosi na jumanne, yakihusisha makundi ya wanamgambo ambao hata hivyo hawakufahamika mara moja. 

Hali ya wasiwasi na taharuki uliikumba miji ya Bossembele na Bossangoa iliyoko umbali wa kilometa  150 kutoka mji mkuu wa Bangui kutokana na machafuko hayo yaliyosababisha mamia ya raia kukosa makazi. 

Hapo jana timu ya maafisa wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR waliwasili katika mji wa Bossangoa kwa ajili ya kutathmini hali jumla ya mambo.

Mashirika ya Umoja wa Mataifa  OCHA, UNICEF, UNFPA, WFP yanatazamia kutuma wajumbe wake kwa shabaha hiyo hiyo ya kutathmini hali jumla ilivyo.

Adrian Edwards ni maemaji wa UNHCR