Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ataka demokrasia kuchukua mkondo wake Maldives

Ban ataka demokrasia kuchukua mkondo wake Maldives

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema anafuatilia kwa makini hali nchini Maldives kufuatia awamu ya kwanza ya uchaguzi Septemba 7 mwaka huu.

Katika taarifa yake iliyotolewa mjini New York Bwana Ban amesema awamu ya kwanza ya uchaguzi ilitambuliwa na waangalizi kimataifa na kitaifa kwa mafanikio .

Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amewataka viongozi wote wa kisiasa kuchukua majukumu yao kwa kuheshimu mchakato wa kidemokrasia ili amani , ujumuishwaji na hadhi ya kura itendeke katika awamau ya pili ya uchaguzi wa raiis September 28 kama ilivyopangwa kwa mujibu wa katiba.

Bwana Ban amesisitiza umuhimu wa kuheshimu utashi wa watu wa Maldives katika mchakato mzima.