Demokrasia imepiga hatua, juhudi zaidi zinahitajikai :UM

19 Septemba 2013

Licha ya machafuko ya mara kwa mara, Afghanistan imepiga hatua kijamii na mahusiano ya kimataifa na juhudi zaidi zinahitajika katika  taifa hilo linapoelekea katika uchaguzi mkuu mwakani.

Akizungumza wakati wa kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililojadili hali nchini humo, mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan Jan Kubis amesema nchi hiyo imepiga hatua katika ujenzi wa mahusiano ya kimataifa na kufafanua namna uelewa wa watu juu ya changamoto na fursa unavyokuwa akisema

(Sauti ya Kubis)

"Katika ukanda kuna kukua kwa utambuzi wa mahusiano ya kimataifa na Afghanistan, changamoto za asili ikiwemo kukosekana utulivu, ugaidi, kukosa makazi, na mihadarati na pia fursa zilizopo kama vile miundombinu na kuungamanishwa yanaonekana kueleweka."

 Amesema maandalizi ya uchaguzi mkuu mwakani mwezi April nchini humo yameonyesha matumaini ya kukua kawa demokrasia Afghanistan huku wajumbe wengine wa mkutano huo wakitaka wanawake washirikishwe kikamilifu katika mchakato huo wa kisiasa.

Akizungumza katika mkutano huo Rais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Gary Quinlan amesema mchango wa jumuiya ya kimatifa kwa usalam endelevu kwa usalama endelevu Afghanistan ni muhimu na kuzungumzia umuhimu wa uchaguzi huru na haki.

(Sauti ya Quilan)

"Jumuiya ya kimatifa kuendelea la kusaidia vikosi vya jeshi na polisi la Afghanistan ni muhimu kwa usalama endelevu wa nchi, kumekuwa na hatua katika mkataba wa Tokyo hatua zaidi zianahitajika. Uchaguzi wenye heshima, jumuishi na uwazi ni muhimu kwa ajili ya mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi."