Nchi 172 kushiriki kongamano la nne la kukabiliana na utumiaji madawa kwenye michezo

19 Septemba 2013

Kongamano la nne la vyama kwa ajili ya kukabiliana na vitendo vya matumizi ya dawa za kuongeza mguvu kwenye michezo hufanyika kila baada ya miaka mine, na hii ni kulingana na mwongozo uliowekwa na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na elimu, sayansi na utamaduni UNESCO.

Kongamano hilo ambalo hufanyika makao makuu ya UNESCO Paris, linajukumu la kuhakikisha kwamba maazimio ya kimataifa ya kukabiliana na vitendo vya matumizi ya dawa kwenye michezo yanatekelezwa.

Wajumbe kwenye kongamano hilo hubadilishana mawazo pamoja na kuendesha mijadala inayoangazia sera ambazo maalumu kukabiliana na wimbi la matumizi hayo.

Hadi sasa jumla ya nchi 174 zimeridhia azimio hilo la kimataifa na tayari nchi hizo zimealikwa kuhudhuria kongamano la nne lijalo litakalofanyika huko Paris, Ufaransa.