Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Fursa za kibiashara, madawa na teknolojia zitasaidia kufikia malengo ya umasikini:UM

Fursa za kibiashara, madawa na teknolojia zitasaidia kufikia malengo ya umasikini:UM

Ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu hatua zilizopigwa kufikia malengo ya maendeleo ya milenia ya kutokomeza umasikini inasema hatua zimepigwa katika nchi zinazoendelea kwa upande wa teknolojia, masoko ya nje, upatikanaji wa madawa na kupunguza mzigo wa madeni lakini jumuiya ya kimataifa inatakiwa kuongeza msaada na kufikia muafaka wa kibiashara. Joseph Msami na maelezo zaidi

(RIPOTI YA JOSEPH MSAMI)

Akizungumza katika uzinduzi wa ripoti hiyo Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amesema malengo ya milenia yamechagiza hatua kutoka kwa serikali , jumuiya za kiraia na wadau wengine kote duniani na kuleta matokeo mazuri.

Amesema kila pembe ya dunia ukiangalia kuna mafanikio katika kufikia malengo hayo ingawa siyo kwa asilimia mia moja. Ripoti hiyo iliyopewa jina “Ushirikiano wa kimataifa kwa maendeleo: changamoto zinazotukabili” Inafuatilia utekelezaji wa lengo la maenmdeleo ya milenia nambari 8 aambalo linahusu ushirikiano wa kimataifa kwa ajili ya maendeleo ukijumuisha suala la misaada, biashara, upunguzaji mzigo wa madeni, fursa za upatikanaji wa madawa muhimu na fursa za teknolojia.