Baraza Kuu latakiwa kuchukua hatua kuhakikisha amani inapatikana

19 Septemba 2013

Mtaalamu huru wa Umoja wa mataifa katika kuchagiza demokrasia na utulivu wa kimataifa Alfred de Zayas Alhamisi amelitaka baraza kuu la Umoja wa mataifa kuchukua jukumu muhimu la kuleta na kulinda amani.

Pia ametaka jukumu makini zaidi kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Matauifa katika kutoa onyo na hatua za haraka kusuluhisha mivutano katika baraza kuu na baraza la haki za binadamukamainavyofafanua ripoti ya Jason Nyakundi

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Katika kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Amani, Bwana Alfred de Zayas amesema kuwa Umoja wa Mataifa ndilo tumaini la kipekee la kumkinga mwanadamu  kutokana na vifo vya kiholela, uharibifu  na kuhama.

Amesema kuwa umetimia wakati ambapo baraza kuu la Umoja wa Mataifa kama mawakilishi wa dunia nzima linastahili  kukataa kabisa na kulaani vita. Amesema kuwa ni jukumu la kila mmoja kuzikumbusha serikali kuhusu wajibu wao wa kutatua tofauti zao kwa njia ya amani na kufanya majadiliano kuambatana na mwongozo wa Umoja wa Mataifa. Bwana de Zayas amesema kuwa hivi majuzi kumekuwa na hatari baada kushuhudiwa vitisho vya matumizi ya nguvu jambo ambalo liko nje ya makubaliano ya Umoja wa Mataifa hali ambayo ingesababisha maafa zaidi.