Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Majaji wa ICC waitaka serikali ya Marekani kumkamata Rais Bashir

Majaji wa ICC waitaka serikali ya Marekani kumkamata Rais Bashir

 

Kufuatia habari kuwa huenda Rais Omar Al Bashir wa Sudan akasafiri hadi Marekani kwa ajili ya mkutano wa viongozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, imetoa ombi kwa mamlaka za Marekani kumkamata Bwana Bashir na kumwasilisha kwa mahakama hiyo iwapo ataingia kwenye eneo la nchi hiyo.

 

Mahakama hiyo pia imeikumbusha Marekani kuhusu waranta mbili za kutaka Bashir akamatwe kwa makosa ya mauaji ya kimbari, uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu.

 

Mnamo Machi 6 2009, Mahakama ya ICC ilitoa ombi ilitoa ombi kuwa Rais Bashir akamatwe na kusalimishwa kwa nchi wanachama wote wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambao si wanachama wa Mkataba wa Roma ambao uliiweka mahakama hiyo, ikiwemo Marekani.