UNESCO yadhibitisha uporaji wa makumbusho ya Mallawi Misri:

18 Septemba 2013

 

 

Ujumbe wa wataalamu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO nchini Misri umethibitisha kwamba karibu kila kitu cha makumbusho ya taifa ya Mallawi yaliyoko Minya, Kaskazini mwa Misri yameporwa wakati wa machafuko ya mwezi Agost.

 

Ujumbe uliotayarishwa na wizara ya mambo ya kale ya Misri na uongozi wa Minya wamebaini kwamba wakati jingo la makumbusho halijaharibiwa saana vitu 600 vya ukusanyaji wa makumbusho kati ya 1080 vimeibibwa.

 

Wataalamu wa kimataifa na mhandisi wa UNESCO Pierre-André Lablaude , pamoja na mtaalamu wa UNESCO wamezuru makum,busho mengine yaliyoharibiwa , hasa matatu ambayo ni makanisa ya kihistoria the Evangelical Church Minya; Amir Tadros Monastery Fayoum; na the Franciscan Sisters School in Beni Suef. Makanisa mengine wameshindwa kuyatembelea kwa sababu za kiusalama.