Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto wakimbizi wa Syria walioko Iraq wasaidiwa vifaa vya shule

Watoto wakimbizi wa Syria walioko Iraq wasaidiwa vifaa vya shule

Wakati sintofahamu ikiendelea kuikumba Syria kufauatia machafuko yanayoendelea kwa takribani mwaka wa tatu sasa, hali ya kielimu kwa watoto ni mabya  wakati huu ambapo taarifa zinasema shule nyingi nchini humo ni makazi ya wakimbizi huku nyingine zikibomolewa.

Lakini kuna habari njema kwa watoto walioko katika kambi ya wakimbizi nchini Iraq ambapo wamepatiwa msaada wa vifaa vya shule ili kuwawezesha kielimu. Ungana na Asumapta Massoi katika taarifa ifuatayo inayofafanua zaidi.