Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chad yaapa kuangamiza njaa na kuongeza mazao ya kilimo:UNDP

Chad yaapa kuangamiza njaa na kuongeza mazao ya kilimo:UNDP

Taifa la Chad litajikita kwenye mpango wa kupambana na tatizo la ukosefu wa chakula kwa kuangazia zaidi malengo ya maendeleo ya milenia, taifa ambalo hadi asilimia 25 ya wenyeji wake huenda wakakabiliwa na njaa huku zaidi ya thuluthi moja ya watoto wakiwa na utapiamlo. Jason nyakundi na taarifa kamili.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Mkuu wa Shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP Hellen Clark  amesema kuwa Chad ina uwezo wa kuafikia uzalishaji wa juu wa chakula na kuwahakikishia lishe watu wake na chakula kilicho nafuu. Bi Clark ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa mpango huo alioufanya na Waziri mkuu wa Chad Djimrangar Dadnadji. Ukiwa utachukua kipindi cha miaka mitatu mpango huo ambao utagharimu dola bilioni moja utazishirikisha serikali katika kutambua njia zinazoweza kusaidia kutatua suala la kutokuwepo usalama wa chakula. Mpango huo utaangazia  kilimo cha unyunyizaji, kuhakikisha kuwepo kwa mbegu na mbolea na vifaa kwa vya kilimo kwa wakulima wadogo huku wanawake wakingaziwa zaidi.Chadimekabiliwa na uhaba wa chakula wa mara kwa mara tangu miaka ya 1970 kutokana na ukame , mafuriko , janga la nzige na mizozo.