Mke wa Rais wa Uganda aongeza juhudi za ahadi ya vita dhidi ya ukimwi:

18 Septemba 2013

Mke wa Rais wa Uganda Bi Janet K Museveni, amedhihirisha juhudi zake za kukomesha maambukizi mapya ya virusi vya HIV kwa watoto kwa kupeleka kampeni ya kitaifa katika eneo la Karamoja, moja ya mikoa isiyojiweza katika nchi hiyo.

Bi Musevern amezindua kampeni ya “kutokomeza maambukizi ya HIV toka kwa mama kwenda kwa motto” Septemba 16 mwaka huu katika mji wa Moroto.

Kampeni hiyo ni sehemu ya jitihada za serikali za kuzuia maambukizi ya HIV miongoni mwa watoto kwa kuchagiza matumizi ya dawa za kufubaza virusi vya HIV kwa kina mama wajawazito ambao wanaishi na virusi. Kampeni hiyo inakwenda sambamba na utekelezaji wa maagizo ya shirika la afya duniani WHO .

Mkurugenzi wa UNAIDS Michele Sidibe akisifu juhudi hizo amesema ukimwi unaweza kudhibitiwa na Afrika inaweza kupata matibabu, kwani juhudi zinafanyika kwa ujasiri, uongozi imara na ushirikiano.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter