UNICEF, Ethiopia wapunguza vifo vya watoto

17 Septemba 2013

Zikiwa zimesalia chini ya siku 1000 kufikia ukomo wa malengo ya maendeleo ya mileni mwaka 2015, nchi kadhaa zinahaha kutimiza malengo hayo manane yaliofikiwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa mwaka 2000.

Makala ifuatayo inaangazia namna Ethiopiailivyopiga hatua katika kupunguza lengo la nne

la kupunguza vifo vya watoto walioko chini ya umri wa miaka mitano.

Ungana na Joseph Msami.