Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu wenye ulemavu ni wahanga waliosahaulika katika vita vya Syria:

Watu wenye ulemavu ni wahanga waliosahaulika katika vita vya Syria:

Vita nchini Syria vinasababisha watu wenye ulemavu kukabiliwa na ukiukaji mkubwa wa haki zao kila siku na wanahitaji kupewa ulinzi mkubwa imesema kamati ya Umoja wa Mataifa ya haki za watu wenye ulemavu CRPD.

Kamati hiyo yenye wataalamu huru 18 imesema kuishi katikati y mgogoro kuanaathiri mwili na akili na hali inakuwa mbaya zaidi kwa watu wenye ulemavu kwani changamoto zao ni kubwa zaidi.

Tume hiyo imesisitiza kwamba Syria imeridhia mkataba wa haki za watu wenye ulemavu hivyo ina wajibu wa kuwalinda chini ya sheria haki za binadamu za kimataifa kwa kutumia kila njia iwezekanayo kuhakikisha usalama wao. Imezitaka pande zote katika mgogoro wa Syria kuacha kuwalenga wananchi na lazima kuchukua tahadhari kuepuka vifo au majeruhi kwa raia. Kamati hiyo inawajibika kufuatilia utekelezaji wa mkataba wa walemavu.

Kamati imeongeza kuwa ni muhimu kwa mmashirika ya misaada ya kibinadamu kuruhusiwa kufanya kazi yao bila vikwazo nchini Syria ili kuwafikishia msaada watu wenye ulemavu wa kabla na baada ya vita ambao wanahitaji msaada huo, na huduma za afya ni lazima zipatikane kwa watu wote wakiwemo wenye ulemavu. Kamati pia imeelezea hofu yao kubwa dhidi ya watu wenye ulemavu waliokimbia machafuko na sasa kuishi kwenye kambi za wakimbizi katika nchi jirani.