Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Raia wa Korea Kaskazini wasema walikumbana na mateso nchini mwao: Kirby

Raia wa Korea Kaskazini wasema walikumbana na mateso nchini mwao: Kirby

Ushahidi uliokusanywa na tume ya uchunguzi juu ya hali ya haki za binadamu huko Korea Kaskazini unaonyesha mazingira ambayo serikali ilihusika kuvunja haki za binadamu. Katika ripoti yake kwa Baraza la Umoja wa Mataifa la haki za binadamu tume hiyo imesema makumi ya raia wa Korea Kaskazini walioko uhamishoni walijitokeza kwa wingi  kutoa maoniyaowakati walipokuwa katika miji yaSeoulnaTokyo. Ushahidi huo uliotolewa kwa faradha na hadharani unaonyesha namna mamlaka za Korea Kaskazini zinavyohusika kwenye matukio ya utesaji, unyanyasaji wa kijinsia na kuwaweka kizuizini raia bila maelezo. Mwenyekiti wa Kamishna hiyo Michael Kirby amesema kuwa wamepata maelezo yanayofahamisha juu ya kuwepo kwa uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu katika maeneo ya magereza.  Raia wengi walioko kwenye vizuizi wanaelezwa kwamba hawana fursa ya kupata chakula na baadhiyaowanakabiliwa na matatizo ya ukosefu wa chakula.

(SAUTI YA MICHAEL KIRBY).

“Tumesikia kutoka kwa watu wa kawaida ambao wamekabiliana na mateso na kutupwa gerezani ambako hakuna walichokifanya mbali ya kuangalia tu tamthilia za nje ama kuwa na vitabu vya imani za dini zao.Wanawake na waume ambao walizingatia kutekeleza haki zao za kibinadamu waliamuliwa kuondoka Korea waliezea mazingira magumu ya mateso waliyokumbana nayo.

Hata hivyo serikali ya Korea Kaskazini imesema haitambui tume hiyo na amewakatalia watumishi wake kuingia nchini humo