Mtawa kutoka DRC kutunukiwa tuzo ya kimataifa ya wakimbizi

17 Septemba 2013

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR limesema kuwa tuzo ya mwaka huu ya Nansen inakwenda kwa mtawa Angelligue Namaika ambaye amekuwa akifanya kazi katika maeneo ya mbali Kaskazini mwa Jamhuri ya Congo akiwahudumia waathirika kwa matendo ya kikatili yaliyofanywa na wapiganaji wa kundi la Lord Resistance Army LRA.George Njogopa anaripoti

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Mtawa Angélique Namaika, ambaye katika mpango wake wa kuunganisha na kuendeleza anaelezwa kuwa ameyanusuru maisha ya zaidi ya watu 2,000 wengi wao ni wanawake na watoto ambao wamelazimika kukimbia makwao na wengine kukubwa na vitendo vya unyanyasaji kutoka kundi la wapiganaji wa LRA.

(Sauti ya Mtawa Angelique)

Wengi ya hao aliowasaidia wamekuwa wakielezea matukio yaliyokumbana nayo ikiwemo yale ya kutekwa, kutumikishwa katika kazi, kupigwa, kuuliwa na vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu. Mbinu yake ya ana kwa ana imewasaidia wengi waliokuwa wakikabiliwa na matizo ya woga na hofu ya maisha. Anaelezwa kwamba amewajengea uwezo wa kujiendeleza kielimu na kuwapa msaada wa kujiingiza kwenye shughuli za ujasiriamali