Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uganda yaonya wanaotumia vyandarua kwa shughuli za uvuvi na ujenzi

Uganda yaonya wanaotumia vyandarua kwa shughuli za uvuvi na ujenzi

Nchini Uganda, katika jitihada za kufikia Malengo ya Maendeleo ya Millenia hususan udhibiti wa vifo kwa watoto na wajawazito vitokanavyo na Malaria, Waziri wa Afya amewaagiza viongozi wa mitaa kumkamata mtu  yeyote atakayekutwa akitumia vyandarua kwa matumizi mengine kando ya kujikinga na mbu. John Kibego wa radio washirika ya Spice FM hukoUgandaana taarifa kamili.

(Taarifa ya Kibego)

Agizo hili limetolewa wakati ambapo serikali inasambaza bure, vyandarua milioni ishirini na moja vilivyonunuliwa kwa ufadhili kutoka miradi mbali mbali ukiwemo ule wa kupambana na malaria wa rais wa Marekani, na wa DFID. Juu ya visa vya vyandarua kutumiwa kinyume na makusudio hapa na pale, kuna hofu kuwa huenda hivi pia visitumiwe kukingia watu kuumwa na mbu. Watu wa Ziwani, wanavitumiakamanyenzo za uvuvi na kwa wengine ni nyenzo za kujenga mabafu. Lakini sasa waziri wa Afya ya Msingi Sarah Opendi anasema serikali haitowavumilia.

(Sauti ya Sarah Opendi)

Kwa upande wake Daktari Jesca Nsungwa, Kamishina Msaidizi wa Huduma za Afya ya Msingi, ameyapongeza Shirika la Afya Duniani - WHO na UNICEF kwa msaada wao katika kupambana na magonjwa yanaokingikakamamalaria na kuhara.

(Sauti ya Daktari Jesca  Nsungwa)