Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IAEA yaanza mkutano mkuu wa 57 Vienna

IAEA yaanza mkutano mkuu wa 57 Vienna

Zaidi ya wajumbe 2000 kutoka nchi 159 wanachama wa shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA wanakutana wiki hii mjini Vienna kwenye kituo cha kimataifa katika mkutano wa 57 wa kila mwaka wa shirika hilo.

Akifungua mkutano huo wa siku tano mkurugenzi mkuu wa IAEA Yukiya Amano ameelezea mafanikio ya liyofikiwa na shirika hilo kwa mwaka uliopita pamoja na changamoto walizokabiliana nazo.

Bwana amino pia ametanabaisha kuhusu miradi ya baadaye ya IAEA ambayo inajumuisha ukarabati wa maabara za nyuklia karibu na mji wa Vienna

(SAUTI YA YUKIYA AMANO)