Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Homa ya mafua ya ndege bado ni tishio: FAO

Homa ya mafua ya ndege bado ni tishio: FAO

Shirika la kilimo na chakula duniani, FAO limetoa taarifa mpya inayoonya kuwa homa ya mafua ya ndege aina ya H7N9 na H5N1 bado ni tishio duniani na kuitaka jumuiya ya kimataifa kuchukua tahadhari. FAO imesema kuna uwezekano virusi hao kujitokeza tena katika kipindi cha msimu wa mafua ya ndege. George Njogopa na taarifa kamili.

(Taarifa ya George)

Onyo hilo limetolewa wakati Afisa Mwandamizi wa Mkuu FAO  Juan Lubroth alipokuwa na mkutano wa pamoja na maafisa wa shirika la misaada la Marekani USAID), shirika la Afya Ulimwenguni WHO na shirika linalohusika na afya za wanyama OIE.

Ili kukabiliana na tatizo hilo la virusi vya mafua ya ndege, FAO imesema kuwa iko tayari kutenga kiasi cha dola milioni 2 ikiwa ni sehemu la nyongeza ya dola milioni 5 zilizotolewa na USAID.

Taarifa hiyo pia imeelezea namna dunia ilivyokuwa tayari kukabiliana na ugonjwa huo wa mafua ya ndege na imewatolea mwito wananchi kuanza kuchukua tahadhari za mapema.

Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Mkuu wa kitendo cha maabara wa FAO mwenye makao yake hukoAustralia, maafisa kutoka China na Marekani.