Valarie Amos ahitimisha ziara Iran na kuzungumzia ushirikiano muhimu

16 Septemba 2013

Mratibu wa Umoja wa mataifa wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura  Bi. Valerie Amos amehitimisha ziara ya siku tatu nchini Iran Jumapili na kukaribisha fursa ya kufanya kazi pamoja na taifa hilo kikanda na katika masuala ya kimataifa. Mratibu huyo amesema Iran ina mfumo mzuri saana wa kujiandaa na kukabili majanga na mara nyingi wanashirikiana uzuoefu huo na uwezo wake wakati wanapokabiliana na hali ya dharura katiika nchi nyingine. Ameongeza kuwa amefdurahi kutia saini taarifa ya pamoja na serikali ya Iran ya kuimarisha ushirikiano baina ya pande hizo mbili na kuboresha uhusiano wa kikanda maktika masuala ya misaada ya kibinadamu. Wakati za ziara yake Bi Amos ameklutana na waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Dr Zarif , Rais wa shirika la kitaifa la kukabiliana na majanga  Bwana Ghaddami na naibu waziri wa mambo ya ndani Dr Farhadi wakiwemo pia jumuiya ya Iran ya chama cha msalaba mwekundu , maafisa wengine wa serikali, wawakilishi wa kibalozi, jumuiya wa watoa misaada ya kibinadamu na mashirika yasiyo ya kiserikali. Bi Amos amesema ushiriki wa Iran ni muhimu hasa wakati huu ambapo jumuiya ya kimataifa inakabiliwa na migogoro mikubwa na yenye tashwishi kwenye kanda na kwingineko duniani. Amewashuruku watu wa Iran na nchi hiyo kwa kuwahifadhi maelfu ya wakimbizi kutoka Iraq na Afghanistan na ameitolea wito jumuiya ya kimataifa kuendelea kusaidia juhudi za Iran na Afghanistan ili kupata suluhishio la ku7dumu la wakimbizi wa Afghanistan.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter