Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tume ya uchunguzi wa matumizi ya silaha za kemikali Syria yakabidhi ripoti kwa Ban:

Tume ya uchunguzi wa matumizi ya silaha za kemikali Syria yakabidhi ripoti kwa Ban:

Ripoti ya tume ya Umoja wa Mataifa ya kuchunguza madai ya matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria imekabidhiwa Jumapili Septemba 15 kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.  Aliyekabidhi ripoti hiyo ni Professor Ake Sellström, anayeoongoza tume hiyo, na Katibu Mkuu ataiwasilisha ripoti hiyo Jumatatu asubuhi kwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa.  Jumatatu ripoti hiyo itawasilisha katika kikao maalumu cha faragha cha baraza la usalama na baada ya kutolewa taarifa hiyo kwa baraza la usalama na baraza kuu la Umoja wa Mataifa Katibu Mkuu atazungumza na waandishi wa habari.