UM wakaribisha makubaliano Somalia, walaani shambulizi.

13 Septemba 2013

                     

Baraza la usalama la Umoja wa mataifa limekaribisha makubaliano ya hivi karibuni kati ya serikali ya Somalia na utawala wa Juba na kupongeza serikali za Ethiopia, jumuiya ya maendeleo ya IGAD, Muungano wa Afrika AU, na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia UNSOM kwa wajibu wao katika kuwezesha majadiliano .

Katika taarifa ya baraza hilo iliyotolewa mjini New York Ijumaa kufuatia taarifa kwa baraza hilo iliyowasilishwa na mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Nicholas Kay, wajumbe wa baraza la usalama wamesisitiza umuhimu kwa pande zote kutekeleza makubaliano, kuepusha vitendo vinavyoweza kuzorotesha usalama , amani pamoja na kusisitiza heshima ya uhuru , utaifa, uhuru wa kisiasa, mipaka na umoja wa Somalia. 

Wajumbe hao pia wamelaani vikali  shambulio lililofanywa  na kundi lenye msimao mkali la Alshabaab  Septemba saba mwaka huu mjini Mogadishu na jaribio la mauaji la Septemba 12 mjini Kismayo na kutoa salamu za rambirambi kwa waathirika wa matuko hayo na jamaa zao. Baraza la usalama limepongeza vikosi vya muungano wa Afrika ,AMISOM, Ethipoia  na jeshi la nchi hiyo kwa kazi ya usalama nchini Somalia na kuvitaka kuendeleza mapambano dhidi ya Al- Shabaab huku wakisisitiza uungwaji mkono wa kifedha wa vikosii hivyo kupitia mfuko wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya AMISOM.

Kuhusu haki za binadamu, taarifa inasema wajumbe wamekaribisha uamuzi wa serikali yaSomaliakuimarisha hali ya haki za binadamu na kuelezea kusikitishwa kwao na taarifa ya uvunjwaji wa haki za binadamu nchini humo ikiwamo ukatili wa kingono na kijinisia na ukiukwaji wa haki za watoto.

Wameitaka serikali kuwachukulia hatua wahusika wa ukiukwaji wa haki za binadamu na sheria za kimataifa za binadamu. Baraza hilo kadhalika  limekaribisha ahadi ya viongozi wa Somalia ya kutafuta mshikamano miongoni mwa watu na jumuiya kimataifa,  ujenzi wa taasisi za kitaifa na uwezo ikiwa ni sehemu ya mkutano kati ya Jumuiya ya Ulaya na nchi hiyo.

Wakati huo huo wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wameelezea wasiwasi wao kuhusu hali mbaya ya kibinadamu inayoendelea katika taifahilona kutaka misaada na usaidizi kwa mamilioni ya wasomali wanaoishi katika mazingira hatarishi