Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kufikia malengo ya milenia kuna matumaini licha ya changamoto: Ban

Kufikia malengo ya milenia kuna matumaini licha ya changamoto: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema wasiwasi uliokuwepo miaka Kumi na Tatu iliyopita wakati malengo ya maendeleo ya milenia yanapitishwa, lakini mafanikio yaliyopatikana katika kufikia malengo hayo manane yamewezesha kupambana na umaskini kwa kasi ya kihistoria. Bwana Ban amesema hayo wakati akizungumza katika mkutano wa jukwaa la kimataifa la wanawake mjini New York, Marekani ukiwa na maudhui Kutoka Syria hadi maendeleo endelevu, jukwaa ambalo wajumbe wake ni wake wa mabalozi wanaowakilisha nchi zao kwenye Umoja wa Mataifa. Katibu Mkuu amesema baadhi ya nchi zinaelekea kutimiza malengo yote manane ikiwemo kupunguza vifo vya watoto walio na umri chini ya miaka mitano na kutokomeza umaskini. Hata hivyo amesema bado kuna mataifa kama vile ya Afrika yaliyo kusini mwa Sahara bado yanakabiliwa na changamoto akitolea mfano elimu kwa watoto na kile anachoshuhudia akiwa ziarani kwenye barahilo.

 (Sauti ya Ban)

 “Watoto Milioni 57 hawako shuleni, wanarandaranda mitaani. Kila ninapotembela nchi kama vile huko Afrika nimeona watoto wanarandaranda mitaani au wanacheza, kwanini wako hapo? Wanapaswa wakati huo wawepo shuleni. Hiyo ni dira yetu Lazima wote tuwarudishe shule. Kila siku watoto Elfu 19 wenye umri chini  ya miaka mitano wanakufa kutokana na magonjwa yanayozuilika. Ni lazima tuokoe vifo hivyo vinavyoweza kuepukika.”

 Nelly Niyonzima ni Makamu Mwenyekiti wa jukwaahilona katika mahojiano maalum na idhaa akafafanua mambo ambayo taasisi hiyo inalenga kutimiza kupitia mkutano huo.

(Sauti ya Nelly)