Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuna haja ya kuendesha tathmini ili kujua ya hali ya chakula nchini Syria:WFP

Kuna haja ya kuendesha tathmini ili kujua ya hali ya chakula nchini Syria:WFP

WFP limeeleza  kuwa ni muhimu kufanya tathmini hiyo wakati huu kwa vile imaebainika kuwa tatizo la njaa ni moja ya sababu inayowasukuma raia wengi  kukimbilia nchi za nje. George Njogopa anaeleza

 (RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Katika kipindi cha mwezi Agosti WFP  halikuweza kutathmini juu ya usalama wa chakuka katika maeneo 39 yaliyoko mjini Damascus na vijijini.

 Hali ya upatikanaji wa misaada ya chakula katika maeneo ya Pwani ya Luttakia inaripotiwa kuporomoka kutokana na mapigano yanayoendelea ambayo pia yamesababisha mamia ya raia kukimbia makazi yao.

WFP imesema pia imeingiwa na wasiawasi mkubwa kutokana na kuendelea kuporomoka kwa hali ya kibinadamu katika eneo la Hassakeh,ambako vikosi vya waasi vumezuia shughuli za usambazaji wa huduma za kibinadamu

Kutokana na hali hiyo WFP inakusudia kukusanya kiasi cha dola za Marekani milioni 176 katika kipindi cha mwezi Septemba na Disemba mwaka huu ili kukithi mahitaji yake ya usambazaji misaada ya chakula katika maeneo yaliyoathiriwa na machafuko. Elizabeth Byrs ni msemaji wa WFP

(SAUTI YA ELIZABETH BYRS)