Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Demokrasia bado safari ndefu Afrika lakini kuna matumaini

Demokrasia bado safari ndefu Afrika lakini kuna matumaini

Tarehe Kumi na Tano Septemba ni siku ya demokrasia duniani. Mwaka huu ujumbe ni kuimarisha sauti za demokrasia. Umoja wa Mataifa unasema kuwa lengo la ujumbe huu ni kuangazia mwanga umuhimu wa sauti za wananchi kupitia wao wenyewe na hata wawakilishi wao katika masuala ya kisiasa, kijamii na kiuchumi. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon katika ujumbe wake wa siku hiyo anatoa wito kwa viongozi duniani, kusikiliza, kuheshimu na kuchukua hatua muafaka kwa sauti za wananchi iwe zinatoka moja kwa moja kwa wananchi wenyewe au kupitia wawakilishi wao. Je wigo wa demokrasia uko vipi katika hali ya kawaida? Sauti zinasikilizwa? Viongozi wanawakilisha wananchi? Ungana na Jason Nyakundi katika makala hii.

(MAKALA YA JASON NYAKUNDI)