Bado tume huru ya kimataifa haijaruhusiwa syria:Henczel:

13 Septemba 2013

Rais wa baraza la haki za binadamu mjini Geneva Balozi Remigiusz Henczel amewaandikia waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry na waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergey Lavrov akiwataka kufikiria fursa ya tume huru ya kimataifa kwa ajili ya Syria kufanya kazi yake ambayo hadi sasa haijapatiwa nafasi nchini humo.

Katika barua zinazofanana balozi Henczel ameainisha kazi za tume hiyo huru ya kimataifa kwa ajili ya Syria ambayo ilianzishwa mwezi Agost 2011 na imekuwa ikitoa taarifa kwa baraza la haki za binadamu kila wakati.

Rais wa baraza pia amesisitiza ukweli kwamba tume haijaruhusiwa nchini Syria licha ya wito uliotolewa mara kadhaa na mapendekezo. Ametaka sula hilo lipewe uzito na kujadiliwa na mawaziri hao wawili wkati wa mkutano wao mjini Geneva.