Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti mpya ya wahamiaji yaangazia ustawi wa kundi hilo

Ripoti mpya ya wahamiaji yaangazia ustawi wa kundi hilo

Kwa mara ya kwanza ripoti ya kila mwaka inayohusisha wahamiaji duniani imeangazia ustawi wa kundi hilo ambapo pamoja na mambo mengine inaonyesha kwamba kuna kundi kubwa la wahamiaji kutoka nchi zilizoendelea kwenda zile zinazoendelea huku pia ikiainisha kwamba wale wanaohama kutoka nchi zilizoendelea kwenda zile zilizoendelea wananufaika zaidi. Ripoti hiyo inafuatia utafiti uliofanyika kati ya mwaka 2009 na 2011 uliohusisha nchi 150 duniani na kuratibiwa na shirika la kimataifa la uhamaja IOM pia inaonyesha kwamba wanaohamia nchi zilizoendelea hawana fuara ukilinganisha na maisha ya wazawa wa nchi zao licha ya kunufaika kiuchumi. Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM.

(SAuti ya Jumbe)