Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwezi Agosti umeshuhudia ongezeko kubwa la Wasyria wanaowasili Ulaya:

Mwezi Agosti umeshuhudia ongezeko kubwa la Wasyria wanaowasili Ulaya:

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linasema limeona ongezeko kubwa la Wasyria wanaowasili kwa boti Kusini mwa Italia. Zaidi ya siku 40 zilizopita Wasyria 3,300 wakiwemo watoto 230 waliokuwa peke yao wamewasili pwani ya Sicily na wengine 670waliwasili wiki iliyopita. Zaidi ya boti 30 zimehusika kuwasafirisha watu hao , wengi wakitokea Misri , ingawa wengine walianzia safari yao Uturuki. Adrian Edwards ni msemaji wa UNHCR.

(SAUTI YA ADRIAN EDWARD)

UNHCR inakadiria kuwa zaidi ya Wasyria 4,600 Syrians wamewasili Italia kwa njia ya bahari tangu mwanzoni mwa mwaka 2013 na theluthi mbili ya watu hao wamewasili mwezi Agost pekee.