UM, Marekani, Urusi wajadili mkutano wa pili kuhusu Syria

13 Septemba 2013

Mjumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na nchi za kiarabu kwenye mzozo wa Syria, Lakhdar Brahimi leo amekuwa na mazungumzo na mawaziri wa mambo ya nje wa Marekani na Urusi huko Geneva, kujadili uwezekano wa kuitisha mkutano wa pili wa kimataifa kuhusu amani ya Syria. Jason Nyakundi na taarifa kamili

(Ripoti ya JASON NYAKUNDI)

Wakati wa mkutano huo iliafikiwa kuwa pande hizo tatu zitakutana tarehe 28 mwezi huu mjini New York, kando ya mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa kukubalian kuhusu tarehe kamili ya mkutano huo. Bwana Brahimi amesema kuwa walifanya mazungumzo yenye manufaa na kuahidi kuwa mkutano wa pili wa Geneva utazaa matunda.

(SAUTI YA BRAHIMI)

“Tunatazamia kazi mnayofanya kuhusu silaha za kemikali nchini Syra. Ni muhimu. Pia ni muhimu kwetu sisi ambaoa tunafanya kazi nanyi kujaribu kuufanikisha mkutano wa pili wa Geneva.”

Hata hivyo waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry amesema kuwa matokeo ya mazunguzmo ya sasa kuhusu kuangamizwa kwa silaha za kemikali nchini Syria yatakuwa ajenda kuu kwenye mkutano wa pili kuhusu Syria.

(SAUTI YA KERRY)

“Rais Obama amejitolea kwa kupatikana kawa suluhu kupitia majadilino na tunajua hata Urusi inataka hivyo. Tunafanya bidii kuhakikisha kuwa hilo limefanyika. Sote tumekubaliana kukutana tena mjini New York wakati wa mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa Septemba 28 ili kuona kama itawezekana kupata tarehe ya mkutano huo ambao kwa kiasi kikubwa utaamua kwa siku kadha kuhusu suala la silaha za kemikali. Marais wetu wana wasi wasi kuhusiana na idadi ya vifo na uharibifu, vitendo vya pande zote ambavyo vimechangia kuongezeka kwa wakimbizi, madhara zaidi kwa binadamu na tumejitolea kushirikiana tukiwa na matumani kuwa jitihada hizo zitazaa matunda na kuleta amani na udhabiti kwenye sehemu hiyo inayokumbwa na vita.”

Waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Sergei Lavrov anasema kuwa nchi yake inafanya kazi na shirika linalopinga matumizi ya silaha za kemikali kuhakikisha kuwa suala hili limetatuliwa kwa haraka.

(SAUTI YA LAVROV)

“Ikiwa sasa serikali ya Assad imejiunga kwenye mkataba kuhusu silaha za kemikali tutawaleta wataalmu wetu pamoja na Shirika linalopinga silaha za kemikali vile tulivyokubaliana na Umoja wa Mataifa , kuweka mpango ambao utahakikisha kuwa susla hili limetatuliwa kwa haraka. Urusi , rais wa Urusi tangu kuanza kwa mzozo nchini Syria amekuwa akipendekeza suluhu la amani, tumeunga mkono sana mpango wa muungano wa nchi za kirabu, wanagalizi wa muungano huo, tuliunga mkono mpango wa Kofi Annan, wakaguzi wa Umoja wa Mataifa na sisi ni sehemu ya wale wanaotaka mkutano wa Geneva”