Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ICC yazungumzia mpango wa Kenya kutaka kujitoa

ICC yazungumzia mpango wa Kenya kutaka kujitoa

Kesi inayaowakabili viongozi wa serikali yaKenyaakiwemo Naibu Rais William Rutto pamoja na mtangazaji wa radio Joshua Arap Sang imeanza kusikilizwa huko The Hague nchini Uholanzi.

Kesi hiyo yenye mvuto nchiniKenya, Afrika mashariki, na dunia nzima kwa ujumla inahusisha tuhuma za kuhusika na vurugu baada ya uchaguzi mkuu nchiniKenya mwaka 2007 ambapo zaidi ya watu 1200 walipoteza maisha huku wengine wakipoteza makazi.

Ungana na Joseph Msami katika makala inayofafanua kile kinachosemwa na waendesha mashtaka na upande wa utetezi walipokutana na waandishi wa habari hususan mpango waKenyakutaka kujitoa  ICC