Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuna wasiwasi na operesheni zetu Afrika, lakini DRC kitisho cha M23 kimepungua: Ladsous

Tuna wasiwasi na operesheni zetu Afrika, lakini DRC kitisho cha M23 kimepungua: Ladsous

Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani ndani ya Umoja wa Mataifa Herve Ladsous amesema wasiwasi wao mkubwa wa operesheni zao  hivi sasa uko barani Afrika hususan Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mali na Sudan. Amesema hayo mjiniNew York, Marekani wakati akitoa taarifa ya utendaji wa ofisi yake kwa waandishi kabla ya kuanza kwa mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa baadaye mwezi huu, Bwana Ladsoud amesema

Mathalani kuhusu DRC amesema kwa miezi kadhaa iliyopita hali ilikuwa si shwari lakini hivi sasa kikosi cha ulinzi wa amani cha Umoja wa Mataifa nchini humo, MONUSCO kwa kushirikiana na jeshi la serikali na kikosi maalum cha Umoja wa Mataifa cha kujibu mashambulizi, hali Goma imetangamaa na tishio la M23 limepungua.

(Sauti ya Ladsous)

“Kundi la waasi la M23 limevurugwa na kusukumwa nyuma  hadi kaskazini na kwa sasa halina tena tishio la  moja kwa moja kama ilivyokuwa  hapo awali, iwe katika mji wa Goma au katika kambi za wakimbizi wa ndani au kwa  MONUSCO hiyo ni hatua kubwa sana. Lakini wakati huo huo tunafaa kukumbuka kwamba hali ilivyo mashariki mwa DRC na katika maziwa makuu ni suala la kisiasa , ni muhimu kujaribu kuyapatia suluhu masuala haya ambayo kwa muda mrefu yamekuwa chanzo cha mateso kwa wengi”

Kuhusu Mali amesema hali inaimarika baada ya uchaguzi na Umoja wa Mataifa utaendelea kuimarisha ujumbe wake wa usaidizi nchini Mali, MINUSMA hususan kwa kuhakisha idadi ya walinzi wa amani inafikia ilivyokubaliwa. Amezungumzia piaSudannaSudankuhusu akisema hali inaimarika na  kuzorota, tatizo linatambulika lakini mikutano ya hivi karibuni kati ya viongozi wa Sudan Kusini naSudanimeleta matumaini mathalani usafirishaji wa mafuta, lakini bado kuna masuala kadhaa.

(Sauti ya Ladsous)

“Bado kunasalia badhi ya mambo na suala ngumu kabisa linabakia lile kuhusu Abyei ambako suluhu la uhakika bado halijapatikana, na ombi la upande mmoja kwamba kura ya maoni ifanyike mwezi ujao na harakati zingine kwenye eneo hilo.”