Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi zitekeleze mkataba ili kufikia amani ya kweli DRC: UM

Nchi zitekeleze mkataba ili kufikia amani ya kweli DRC: UM

Rais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Gary Quinlan ameelezea wasiwasi wa wajumbe wa barza hilo juu ya kudorora kwa amani mashariki mwa Jamhuri ya Kimdemokrasia ya Kongo, DRC na hivyo kuzitaka nchi zilizotia saini mkataba wa amani ,usalama na ushirikiano kwa ajili ya DRC na ukanda wa maziwa makuu kutekeleza ahadi zao ili kufikia amani ya kudumu.

Akitoa muhtasari wa kilichojiri katika mkutano wa baraza la usalama leo ambapo wanachama walipokea taarifa kwa njia ya video juu ya hali amani DRC kutoka kwa mwakilishi maalum wa UM katika ukanda wa maziwa makuu Bi Mary Robinson pamoja na mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu katika ukanda huo Martin Kobler, Rais wa baraza la usalama amesema wanapongeza ziara ya pamoja ya wawakilishi hao wa Umoja wa Mataifa, Muungano wa Afrika, Ulaya na Marekani nchini DRC, Rwanda na Uganda iliyofanyika Septemba tatu hadi saba katika juhudi za kuimarisha amani katika ukanda huo.

Kadhaika Quinlan amesema baraza limezingatia maazimio ya mkutano wa saba wa wakuu wa nchi wa ukanda huo uliofanyika jijini Kampla nchini Uganda Septemba tano. Kuhusu msimamo wa baraza anasema

(SAUTI QUILAN)

"Wajumbe wa baraza la usalama walielezea kuunga mkono utekelezaji wa ahadi chini ya mkataba wa amani, usalama na ushirikiano kwa ajili ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo na ukanda mzima na kuwataka nchi wahusika kutimiza ahadi zao kwa nia njema amabyo ni muhimu katik akufanikisha amani endelevu Mashariki mwa DRC na ukanda wa maziwa makuu. Kwa kuzingatia hili wajumbe wa baraza wanautarajia makutano ujao wa uzimamizi wa ukanda utakaofanyika SDeptember 23 mjini New York."