Siku ya kimataifa yaelezea faida za ushirikiano wa Kusini-Kusini:

12 Septemba 2013

Alhamisi ya leo Umoja wa Mataifa unasherehekea jinsi nchi zinazoendelea zinavyotegemeana na kushirikiana utaalamu, ujuzi na taarifa katika kushughulikia matatizo kama umasikini na njaa.

Siku ya Umoja wa Mataifa ya ushirikiano wa Kusini-Kusini inaadhimishwa wakati juhudi za kimataifa zikiongezeka kufikia malengo ya maendeleo ya milenia ifikapo 2015.

Rebecca Grynspan, ni msimamizi mwandamizi wa shirika la Umoja wa mataifa la maendeleo UNDP , ametoa ujumbe maalumu wa siku hii kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa.

(CLIP OF REBECCA GRYNSPAN)

"Ushirikiano wa Kusini –Kusini unatoa suluhu muafaka kwa changamoto za maendeleo. Kushirikiana Kushirikiana uzoefu, kufadhili miradi ya majaribio,kutoa mitaji ya kuboresha miradi, kusambaza bidhaa za kikanda, kuanzisha na kutumia tekinolojia  muafaka, hizi ni fursa ambazo jumuiya ya kimataifa inapaswakuziinua."

Mijadala mbalimbali inafanyika kwenye Umoja wa Mataifa kuadhimisha siku hii ,ukiwemo ule wa utekelezaji wa mipango endelevu ya ulinzi wa kijamii.