Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Japan yaokoa wenye njaa Zimbabwe

Japan yaokoa wenye njaa Zimbabwe

Huko Zimbabwe ukosefu wa uhakika wa chakula miongoni mwa familia maskini umepata ahueni baada ya Japan kulipatia shirika la mpango wa chakula duniani, WFP dola Milioni Nne nukta Mbili kuimarisha upatikanaji wa chakula na lishe bora. Alice Kariuki anafafanua zaidi.

 (RIPOTI YA ALICE KARIUKI)

Msaada huo wa Japan unakuja huku kukiwa na tishio la usalama wa chakula katika eneo la Kusini mwa Afrika. Kiasi cha watu milioni 2.2 watakuwa na mahitaji ya chakula katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Machi mwakani.

Takwimu hizo ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa hivi karibuni ambao ulihusisha serikali ya Zimbabwe na Umoja wa Mataifa. Fedha zilizotolewa na Japani zitaendeleza miradi inayoratibiwa WFP ikiwemo ile inayohusu familia maskini. WFP ikishirikiana na washirika wake imeanza kuandaa mpango ambao utahakikisha kuwa familia zaidi ya milioni 1.8 zilizo katika hali mbaya zinafikiwa na msaada wa awali.