Watembea Arusha hadi Dar es Salaam kunusuru wanyamapori

12 Septemba 2013

Nchini Tanzania, juhudi za kukabiliana na wimbi la ujangili wa wanyamapori zimeanza kushika kasi kufuatia kampeni iliyoanzishwa na makundi ya kiharakati ambayo leo yamehitimisha safari ya kutembea kwa miguu kutoka Mkoani Arusha hadi jiji Dar es salaam. Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa zaidi ya tembo 17,000 waliuaawa katika kipindi cha mwaka 2011 na kuna uwezekano idadi hiyo pengine ikawa kubwa ya hiyo. Kutoka dsm George Njogopa anaarifu zaidi.

(Ripoti ya George)

Kufanyika kwa juhudi hizo kunafuatia ongezeko kubwa la vitendo vya uwindaji haramu ambao unatishia mustakhabali jumla wa wanyamakamatembo na twiga. Ripoti zinasema kwamba kukua kwa  biashara ya pembe za ndovu katika nchi zaasiana barani Ulaya ndiko kunakosukuma makundi ya kijangili kuvamia misitu ya kiafrika. Wanaharakati hao ambao wamesafiri umbali wa zaidi ya kilometa 600  wametuma ujumbe wakitaka kukomeshwa kwa vitendo hivyo. Mmoja wa watembeaji hao ameeleza ugumu wa safari hiyo.

(Sauti)

Baadhi ya wanasiasa pamoja na watetezi wa mazingira wanaitupia lawama serikali kwa kushindwa kuweka mikakati madhubuti kukabiliana na wimbihilola majangili. Akizungumza na idhaa hii kandoni mwa matembezi hayo, Mbunge James Limbeli alisema kuwa.

(Sauti)

Ripoti zinaonyesha kuwa vitendo vya uwindaji haramu vimeshika kasi katika nchi za Afrika ya Kati. Kwa upande wake Naibu Waziri wa Utalii na maliasili Lazaro Nyalandu amesema kuwa  serikali inajua ugumu wa kukabiliana na kadhia hiyo, lakini siku za majingili hao zinaanza kuhesabika

(Sauti)

Idadi ya tembo inaripotiwa kupungua katika mataifa mengi ya afrika, na huko nchini Ivory Cost tembo walioko sasa wanafikia 800. Katika eneo la Kaskazini mwaCameroonkiasi cha tembo waliouliwa na makundi ya waasi kutoka nchi za Chadn aSudanwalifikua 450.NchiniTanzaniahali pia ni mbaya.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter