Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mzunguko wa wakimbizi kuhifadhiana

Mzunguko wa wakimbizi kuhifadhiana

Kumejitokeza kiroja cha mambo kinachohusisha waliokuwa wakimbizi katika nchi Jamhuri ya Afrika ya Kati na wale kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kufuatia kuzuka kwa machafuko katika eneo linalotenganishwa na nchi hizo mbili. 

Kwa hivi sasa kunaripotiwa kuibuka kwa machafuko hayo yaliyohamia katika mto OUbangui ambao unatenganisha nchi zote mbili.

Kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR waliokuwa wakimbizi wa Congo ambao walipewa hifadhi katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, sasa wanajikuta wanachukua jukumu jipya.

Raia hao ambao sasa wamerejea nyumbani Congo wamechukua jukumu la kuwahifadhi wakimbizi wa Jamhuri ya Kati kutokana na machafuko yanayoendelea huko. UNHCR inasema kuwa wakimbizi waliohifadhiwa mwanzo sasa wanajikuta nao wanawahifadhi wale waliotoa hifadhi mwanzo.