Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaalamu wa UM aonya juu ya kuwapuza watu wanaokosa nyumba nchini Uingereza

Mtaalamu wa UM aonya juu ya kuwapuza watu wanaokosa nyumba nchini Uingereza

Mtaalamu maalumu wa Umoja wa Mataifa juu ya nyumba Raquel Rolnik,amesema kuwa ni jambo la kusikitisha kuona mamia ya watu huko Uingerza hawana fursa za kupata makazi bora.

Ameonya juu ya uwekezano wa kutokeza madhara katika siku za usoni iwapo mipango ya serikali haitatoa kipaumbele kwa tatizo hilo. Grace Kaneiya na taarifa kamili:

(RIPOTI YA GRACE KANEIYA)

Mtaalamu huyo amesema kuwa Uingereza imekuwa na historia ya miaka mingi kuwaandalia nyumba bora raia wake na inapaswa kiufanya hivyo wakati wote.

Akizungumza mwishoni mwa ziara yake, amesema kuwa ni muhimu utekelezwaji wa mipango hiyo ikadhihirika kwenye sera.

Ziara hiyo ambayo ni ya kwanza kuifanya, ilikuwa na lengo la kutathmini na kukagua namna ya utekelezaji wa mipango ya inayohimiza makazi bora kwa wote bila ubaguzi. Ziara hiyo inafuatia wito uliotolewa na baraza la haki za binadamu ambalo linapiga marafuku vitendo vya ubaguzi wa makazi.

Akielezea zaidi juu ya makazi bora, Bi Rolnik alisema kuwa mtu kuwa maskini nchini Uingereza haimanishi kwamba anatumbukia kwenye janga la kukosa makazi ama kuishi kwenye nyumba zilizochakaa na mbaya.

Akiwa nchini humo, mtaalamu huyo ametembelea miji ya London, Edinburgh, Glasgow, Belfast na Manchester, ambako alikutana na kufanya majadiliano na maafisa wa serikali wanaofanya kwenye idara za nyumba. Pia alikutana na makundi mengine ya watu.  “