UM wasikitishwa na Venezuela kujitoa katika mkataba wa haki za binadamu.

10 Septemba 2013

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu imeelezea kusikitishwa kwake na hatua ya Venezuela kujitoa katika mkataba wa haki za binadamu wa Marekani.

Akiongea mjini Geneva msemaji wa ofisi hiyo Rupert Colville amesema licha ya kwamba nchi hiyo imejitoa tangu Septemba mwaka jana lakini madhara ya uamuzi huo yanaonekana leo na kusisitiza kwamba uamuzi huo unaweza kuathiri haki za binadamu nchini Venezuela na kwingineko.

Bwana Colville ameisisitiza serikali ya nchi hiyo na mataifa mengine katika barani humo kuendelea kushirikiana na vyombo vya haki za binadamu kikanda na kimataifa na kuzitaka kutochukua hatua yoyote inayoweza kudhoofisha haki za ulinzi wa haki za binadamu akitolea mfano wa kujitoa katika uikanda huo.