William Ruto na Joshua Arap Sang wakana mashtaka dhidi yao huko The Hague

10 Septemba 2013

Huko The Hague hii leo imeanza kusikilizwa kesi dhidi ya William Ruto, Naibu Rais wa Kenya na Joshua Arap Sang, mwandishi wa habari wa kituo kimoja cha Radio. Mbele ya jopo la majaji watatu linaloongozwa na  Jaji Chile Eboe-Osuji kutokaNigeria, William Ruto na Joshua arap Sang walisomewa mashtaka dhidi yao na mwendesha mashtaka Anton Stynberg.

 (Sauti ya Anton)

 Kila mshtakiwa na makosa matatu ya uhalifu dhidi ya binadamu; Mauaji, Kufukuza au kulazimisha watu kuondoka, na utesaji yaliyotendwa katika kipindi cha 30 Disemba 2007 hadi 16 januari 2008. mashata haya yanahusiana na ghasia zilizotendeka katika maeneo manane ya Rift Valley, kwenye wilaya za Wasungishu na Nandi. Upande wa mashtaka utaleta hadi mashahidi Ishirini na Wawili wakiwemo waathirika na mashuhuda, ambao ni raia wa kawaida wa Kenya kuelezea walichoshuhudia kwenye maeneo hayo.”

Wote wamekana mashtaka dhidi yao yanayodaiwa kusababisha vifo vya zaidi ya watu Elfu Moja Mia Mbili na maelfu kupoteza makazi. Wakati huo huo kesi dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta ambaye naye anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu wa kivita kwenye mahakama hiyo ya ICC inatarajiwa kuanza kusikilizwa mwezi Novemba. Huko Kenya  nini maoni ya wananchi wakati huu ambapo kesi hiyo imeanza kusikilizwa?

 (Sauti za wananchi)