Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Saudia imechanga dola milioni 10 kwa wakimbizi wa Kipalestina kutoka Syria

Saudia imechanga dola milioni 10 kwa wakimbizi wa Kipalestina kutoka Syria

Ufalme wa Saudia umeitika wito wa ombi la Syria la msaada kwa ajili ya shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA na kutoa dola milioni 10 kupitia mfuko wa Saudia kwa maendeleo.

Machafuko nchini Syria yanaendelea kuathiri kambi za UNRWA ambayo inakadiria kwamba zaidi ya nusu ya wakimbizi 529,000 wa Kipalestina walioko Syria sasa wamesambaratishwa na machafuko, ama ndani ya Syria au katika nchi jirani zikiwemo Lebanon na Jordan.

Mchango wa Saudia utasaidia juhudi za UNRWA kuendelea kutoa msaada wa chakula na fedha pia msaada wa dharura , huduma za afya na elimu kwa wakimbizi wa Kipalestina. Akikaribisha msaada huo kamishina mkuu wa UNRWA Filippo Grandi amesema katika maeneo ya Syria mbako Wapalestina wengi wanaishi wameshuhudia mapigano makali na idadi ya Wapalestina wanaosambaratishwa ni kubwa na inaongezeka kila siku.