Mgogoro wa Syria umeacha makovu yasiyoonekana kwa watoto:UNICEF

10 Septemba 2013

Kuendelea kushuhudia vita  na machafuko kwa muda mrefu, kutawanywa, kupoteza rafiki zao na familia za na pia kuzorota kwa hali ya maisha kumewaacha watoto wa Syria na makovu ya daiama limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF. Kwa mujibu wa mkurugenzi wa UNICEF kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika Maria Calivis , wazazi wameripoti kwamba watoto wao wanapata majinamizi na kuwa na visirani kila wakati. Pia hali ya watoto kukojoa kitandani imekuwa kawaida ikiambatana na watoto hao kujitenda. Marixie Mercado msemaji wa UNICEF anasema hata piacha zinazochorwa na watoto hao mara nyingi ni za vita na hasira, zikionyesha umwagaji damu , milipuko na uharibifu

(SAUTI YA MARIXIE MERCADO)

‘’Nimeongea na mtaalamu wetu wa kulinda watoto anayefanya kazi kwenye kambi ya Za’atari Jordan asubuhi hii. Amesema jinsi watoto wanavyoelezea ninmi kinachoendelea Syria sasa kinabadilika. Wanazungumzia aina tofauti ya vita, wanazungumzia silaha za kemikali , lakini bila uelewa wa nini wanachokisema.Inaonyesha kwamba watu wazima wanaosikilizwa na watoto hao pia wako katika mtafaruku, na wamekuwa katika hali hiyo kwa muda mrefu na hivyo kushindwa kubagua kile wanachosema mbele ya watoto. Kama tutashindwa kuwarejesha watoto katika hali zao, watashindwa kuwa na uhusiano mzuri na familia zao, na tutapoteza kizazi cha watoto wa Syria ambacho kinajiamini.

UNICEF inakadiria kwamba zaidi ya watoto milioni 4 waSyriawameathirika na vita vinavyoendelea.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter