UM wakaribisha mipango ya kitaifa kupinga ubaguzi wa rangi Mauritania:

9 Septemba 2013

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ubaguzi wa rangi Mutuma Ruteere, amepongeza hatua ya serikali ya Mauritania ya kuanza mchakato wa kuandaa mipango ya hatua za kitaifa dhidi ya ubaguzi wa rangi , lakini ameitaka nchi hiyo kuchambua na kutathimini vipengele vyote vya ubaguzi. Alice Kariuki na taarifa kamili.

Bwana Ruteere akihitimisha ziara yake nchini Mauritania amesisitiza kuwa mchakato wa kuandaa mipango lazima ujumuishe na kushitrikisha pande zote ili kila mtu ajihisi ana wajibu wa kumiliki na kutekeleza.

Akiwa nchi humo amesema ameshuhudia maswali kuhusu ubaguzi na kutengwa yanavyochagiza hamasa na akili za watu na ndio maana amesema ni muhimu kwa wadau wote kubadilishana mawazo na kujadili mipango ya hatua za kuchukua.Kwa mtazamo wake tathmini ya kina haiwezi kufanyika bila takwimu zinazotenganisha uasili, rangi, jinsia na umri, ambazo zimekusanywa kwa watu kutoa maelezo yanayowahusu.

Amesema tawimu hizo ni mkuhimu ili kubaini ni kundi gani linalotengwa na kutathinmini hatua zilizopigwa kushughulikia masuala ya ubaguzi na kutengwa.

Mwakilishi huyo pia ameipongeza Mauritania kwa ushirikiano wake na mfumo wa haki za binadamu wa Umoja wa mataifa , ili kuanzisha tume ya haki za binadamu ya kitaifa , kufanyia katiba mabadiliko,ili kukubali makundi mbalimbali katika jamii na kupitiosha sheria za kupinga masuala ya utumwa. Matokeo ya tathimini na mapendekezo ya mwakilishi huyo maalumu yatajumuishwa kwenye ripoti ya baraza la haki za binadamu mwezi Juni 2014.