Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wa kipalestina wapata makazi mapya bora huko Gaza

Wakimbizi wa kipalestina wapata makazi mapya bora huko Gaza

Zaidi ya wakimbizi 1,200 wa kipalestina wanaoishi Gaza, wamekabidhiwa makazi mapya kwenye eneo la Khan Younis, kufuatia kukamilika kwa mradi wa ujenzi kwenye ukanda wa Gaza,. Mradi huo wa makazi mapya 226 umetekelezwa na Japani kwa ushirikiano na shirika la Umoja wa Mataifa la kusaidia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA.

Mkuu wa operesheni wa UNRWA Robert Turner amesema wanufaika wa mradi huo ni wakimbizi wa kipalestina ambao makazi yao yaliharibiwa kabisa au kubomolewa wakati wa mpango wa Israel wa mwaka 2005 wa kuwahamishia makazi mapya raia wake. Japan ilitoa dola zaidi ya Milioni 12 kusaidia ujenzi huo na shule mbili, kituo cha afya na cha ustawi wa jamii bial kusahau maji na umeme. Shughuli ya kukabidhi makazi hayo ilijumuisha pia Naibu mwakilishi wa Japan huko Palestina Makoto Honda.