Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mipango ya nyuklia ya DPRK na IRAN yatutia hofu: Mkuu IAEA

Mipango ya nyuklia ya DPRK na IRAN yatutia hofu: Mkuu IAEA

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la nishati ya atomiki duniani, IAEA, Yukia Amano amesema bado ana wasiwasi mkubwa na mipango ya nyuklia ya Korea Kaskazini-DPRK na Iran. Amano ameieleza bodi ya magavana wa shirika hilo Jumatatu kuwa wasiwasi wake kuhusu Korea Kaskazini unatokana na taarifa za nchi hiyo kuhusu jaribio la tatu la nyuklia, nia yake ya kuanzisha mtambo wa nyuklia huko Yongbyo, mipango ya awali ya kuboresha Uranium na ujenzi wa kinu kipya cha nyuklia. Amesema hatua hizo zinasikitisha na ni ukiukwaji wa maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Kuhusu Iran amesema…

(Sauti ya Amano)