Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu milioni 774 kote duniani hawajui kusoma na kuandika:UNESCO

Watu milioni 774 kote duniani hawajui kusoma na kuandika:UNESCO

Zaidi ya asilimia 84 ya watu wazima ambao walikuwa hawajui kusoma na kuandika sasa wanaweza kufanya hivyo. Hii ni kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO, kiwango hicho ni ongezeko la asilimia 8 katika kipindi cha kuanzia mwaka 1990.

Hata hivyo UNESCO inasema kuwa bado kuna watu milioni 774 duniani kote ambao hawajui kusoma na kuandika.Takwimu hizo mpya zimetolewa kuambatana na siku ya kujua kusoma duniani itakayoadhimishwa Jumapili hii.Ripoti inasema kuwa Idadi kubwa ya watu wanaokabiliwa na tatizohilowako baraniAsiana Afrika.

 Nchini Tanzania Wataalamu wa sekta ya elimu wanasema hali ni ya kutia matumani na kwamba huenda ikafanikiwa zaidi katika siku za usoni kutokana na mipango ya maendeleo iliyoanzishwa. Basi ungana na George Njogopa ambaye anapiga darubini hali jumla ilivyo.

(MAKALA YA GEORGE NJOGOPA)