Katibu Mkuu wa UM ahimiza kufanyika mkutano kuhusu Syria:

6 Septemba 2013

Kama sehemu ya juhudi zake za kuhimiza kufanyika mkutano kutatua mgogoro wa Syria Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amemkaribisha mwakilishi wa pamoja wa Umoja wa mataifa na Muungano wan chi za Kiarabu kwa ajili ya Syria kuungana naye mjini Saint Petersburg.

Katibu Mkuu yuko kwenye mji huo wa Urusi kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa mwaka huu wa mataifa yaliyoendelea kiuchumi yajulikanayo kama G-20.

Ban amesema mwakilishi huyo wa Syria, Lakhdar Brahimi, sasa yuko njiani kuelekea Urusi ili kumsaidia kuchagiza mkutano wa kimataifa kwa ajili ya Syria.

(CLIP YA BAN KI-MOON)

"Wakati viongozi wanahudhuria mkutano wa G20, kujadili hali ya uchumi duniani , hali iliyosababishwa na madai ya matumizi ya silaha za kemikali na kuendelea kuzorota kwa hali ya kibinadamu Syria vinahitaji haraka viongozi wa dunia kuelekeza ari yao ya kisiasa ili kushughulikia hali hiyo. Na ndio maana nimemuomba mwakilishi wa pamoja Lakhdar Brahimi kuja kujiunga nami Saint Petersburgh kushinikiza kufanyika mapema mkutano wa pili wa Geneva.”

Mkutano wa kwanza wa Geneva kuhusu Syria ulifanyika Juni mwaka jana.